
Amani iwe nanyi nyote popote pale mlipo mkimbizana na maisha.Amani kwenu wote mlio na taabu mbali mbali za kimaisha hasa magonjwa mbalimbali.Amani kwenu na kwangu pia kwa kuwa tu ngali twavuta pumzi ya uhai.
Amani kwenu wote mnayoifikiri nchi yetu Tanzania kwa kuiombea mema na kuitendea mema na Watu wakaao ndani yake.Amani kwa Watanzania halisia sio wale wanaotaka uraia wa Bosnia au Brazil.
Amani kwako Kaka Muhidini Issa Michuzi,Ndesanjo Macha na Wana blogu wote popote pale mwiishipo kwa kujaribu kuwasiliana kwa maneno au kwa picha.
Ninayofuraha ya kipekee kuwakaribisheni nyote kwenye blogu yetu ya Mwisho wa Reli,yaani Blogu tokea Kigoma.Naomba tushirikiana kujenga uelewa wetu kwa kuelimishana pasi kugombana au kutukanana sipendi kutumia neno kupigana kwani ni neno tata na lina Matata zaidi.
Karibuni nyote tuweze kupeana amani ya kifikra na kivitendo kutatua matitizo yanayotuzunguka kwa kusababisha sisi wenyewe au wachache miongoni mwetu kwa makusudi au kwa kutokujua.
Twaweza kugombana kwa hoja zenye akili na sio hoja kwa njia ya matusi kwani haitakuwa suluhisho la matatizo yetu kama jamii.
Kama jamii ya Kitanzania hakuna anayeturoga au anaturoga,toka nje ya sisi wenyewe....na wala sio nchi ya ZE COMEDY...ni nchi halisi na sisi ndio wenye nchi.
AMANI KWENU NYOTE.
No comments:
Post a Comment